1.0 Utangulizi
Kipepeprushi hiki kinatoa maelezo mafupikuhushu namba ya utambulisho ya mlipakodi.Tanzania ilianzisha utaratibu wa kuwatambulisha walipakodi wake kwa kuanzisha Nambari ya Utambulisho
wa mlipakodi au kwa kiingereza “Taxpayer Identification Number” - kwa kifupi TIN. Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 katika kifungu cha 133 inatamka kila mtu aliye na mapato yanayopaswa kutozwa kodi ya mapato ajisajili katika ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania katika muda wa siku 15 tangu kuanza kwa biashara.
2.0 TIN ni nini?
TIN in namba itolewayo kitaalamu kwa teknolojia ya komputa na hivyo kuwa namba ya kipekee isiyoingiliana na namba nyingine. Namba hiyo hupewa mlipakodi na kuwa utambulisho wake katika shughuli zake zote za kibiashara.
3.0 Ni watu gani wanapaswa kujisajili kwa ajili ya TIN?
Watu wote ambao wanastahlili kulipa kodi lakini bado hawajasajili TRA wanapaswa kujisajili na kupewa TIN ili waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi kihalali bila usumbufu. Watu wote wanaoanzisha biashara mpya ajili ya TIN?
4.0 Mtu akitaka kujisajili kwa TIN afanye nini?
Mtu akitaka kujisajili kwa TIN anatakiwa kutembelea ofisi ya TRA ambapo atapewa fomu ya maombi na atajaza na kuambatanisha vitu vifuatavyo. Barua ya utambulisho wa makazi (TIN ya biashara) Kitambulisho cha kudumu kama kadi ya kupigia kura, kitambulisho cha uraia, hati ya kusafiria (pasipoti) na aina nyingine kama itakavyotakiwa. Picha 2 za pasipoti saizi.
Mkataba wa pango la sehemu ya biashara (kama amepanga)
Ikumbukwe: Baada ya kurudisha fomu mwombaji atatakiwa kuchukuliwa alama za vidole (Biometric) na kupigwa picha.
5.0 Je kwa utaratibu huu wa kuchukuliwa alama za vidole mtu anaweza kumuwakilisha mtu mhitaji wa kupata TIN?
Hapana! Kwa utaratibu ulivyo kwa sasa haiwezekani kabisa mtu kumtafutia mtu TIN kwa kumuwakilisha na kuchukua alama za vidole kwa niaba. Kila mwombaji ni lazima afike mwenyewe ofisi ya TRA na kuchukuliwa alama za vidole, utaratibu huu ni ili kuepuka mtu kuwa na TIN zaidi ya moja
6.0.Mtu mwenye TIN anatambulika namna gani?
Mlipakodi aliyesajiliwa hupewa Hati yenye namba ya utambulisho wa Mlipakodi. (TIN Certificate). Hati hiyo hutolewa na Kamishna.
7.0 TIN ina umuhimu wowote?
Ndiyo. Mtu asiye na TIN hana haki, kwa mujibu wa sheria, kupata huduma au shughuli na taasisi zilizoorozeshwa kwenye aya namba 6.0 kama ifuatavyo:
- Kusajili aukubadilisha hati ya kumiliki ardhi,
-Kupata leseni ya udereva,
-Kusajili gari au kuhamisha miliki ya gari,
-Kupata leseni ya biashara na ya viwanda.
-Kusajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT),
-Kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi, au kufanya biashara ya uwakala wa forodha wa kutoa mizigo bandarini.
-Kuingia mikataba, kupata zabuni ya utoaji huduma au bidhaa.
8.0 Taasisi zifuatazo ni lazima kwa mujibu wa sheria zipate nakala ya TIN ya mlipakodi kabla ya kutoa huduma ya kiuchumi kwa mtu yeyote:
-Kamishna wa Ardhi
-Serikali Kuu na Serikali za Mitaa
-Msajili wa magari
-Msajili wa makampuni, majina ya biashara, hakimiliki na alama za biashara
-Wizara ya Viwanda na Biashara
-Kamishna wa Kodi za Ndani
-Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa.
-Wizara zote na wakala zake, Serikali za Mitaa, Mashirika ya Umma,
-Makampuni, Mabenki, Taasisi za Fedha, Vyama vya ushirika na Taasisi za Fedha, Vyama vya Ushirika na Taasisi au vyombo vya Umma,
9.0 TIN ina fada gani kwa Taifa?
Faida kwa Taifa ni kama zifuatavyo:
-Wigo wa kodi utapanuka na kuongeza pato la Serikali.
-Pato la serikali likiongezeka, huduma za jamii na kiuchumi kama vile maji, barabara, afya, elimu, ulinzi n.k zitaboreshwa zaidi.
-Ukwepaji kodi utathibitishwa na hivyo kuongeza ari ya ulipaji kodi kwa hiari na kwa haki.
-Inachochea kukua kwa uchumi kwa kutoa mazingira bora ya ushindani wa haki kibiashara kwa kudhibiti biashara za mifukoni.
-Inarahisisha upashanaji taarifa kati ya idara au taasisi mbalimbali za serikali na hivyo kuboresha huduma na kudhibiti ukwepaji kodi.
10.0 Je kwa utaratibu huu wa kuchukuliwa alama za vidole mtu anaweza kumuwakilisha mtu mhitaji wa kupata TIN?
-Ni walipakodi wenye TIN tu ndiyo watatambulika kama wafanya biashara halali.
-Wenye TIN ndio pekee wanaostahili kumiliki soko la ndani na nje kwa vile ni wao pekee watakaopewa zabuni, leseni, mikopo ya biashara, kandarasi na uingizaji nchini/ ipelekaji nje bidhaa.,
-Wenye TIN wanalindwa na sheria dhidi ya ushindani usiokuwa halali.
11.0 Je, Kuna malipo yoyote yanayotakiwa kufanywa kwa ajili ya kupewa TIN?
Hapana! TIN hutolewa kwa yeyote anayestahili bila malipo yoyote.
12.0 Ni watu gani wasiosahili kujisajili na TIN?
Watu wasiostahili kujisajili ni wale wasio na mapato yatozwayo kodi au waajiriwa ambao mapato yao yote hutozwa kodi kwa mpango wa PAYE. Hata hivyo endapo watahitaji kusajili chombo cha moto TIN itahitajika.
TIN hutolewa bure
“Usitoe Rushwa ili kupata TIN”
“Pamoja tunajenga Taifa letu”
Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali wasiliana na:
Ofisi ya TRA iliyo karibu nawe
Au,
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwaMlipakodi
S.L.P. 11491, Dar es Salaam
Simu: +255 22 - 2119343
Kituo cha huduma kwa wateja:
0786 - 800 000 ( Airtel )
0713 - 800 333 ( Tigo )
0800 - 110 016 Vodacom na TTCL
Barua Pepe: info@tra.go.tz
Tovuti: www.tra.go.tz
Juni, 2014 Toleo la 4
TANZANIA REVENUE AUTHORITY
ISO 9001: 2008 Certified
We pour our heart to global comunity by enlightening social challenges and solve them through a tangible information in all aspects of your life.Make sure you surf our blog frequently for your benefit.
الاشتراك في:
الرسائل (Atom)
-
to see HAPPYDAY MINISTRY TANZANIA BLOG click here
-
Kukiliza bbc swahili radio bonyeza hapa